WATANZANIA TUPINGE USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA
Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.
Lowassa ambaye pia ni
Mbunge wa Monduli, Alisema kuwa ushoga
na hai za ndoa kwa watu wa jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa
nchini.Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.
“Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki,” alisema
Ndoa za mashoga kuhalalishwa Uingereza
Ndoa za watu wa jinsia
moja zitahalalaishwa katika mataifa ya England na Wales, baada ya bunge la
Uingereza kuidhinisha mabadiliko ya mwisho katika sheria ambayo inaungwa mkono
na waziri mkuu David Cameron.
Sheria hiyo
imesababisha mgawanyiko katika chama cha kihafidhina, Conservative, cha David
Cameron. Sheria hiyo inaungwa mkono na vyama vingine wiwili vikubwa nchini
Uingereza, Labour na Liberal Democrats.
Wabunge wa chama cha
Conservative wamepiga kura mara mbili kuipinga sheria hiyo. Mswada wa sheria
hiyo ulipitishwa baada ya mdahalo uliodumu kwa masaa mawili, na inasubiri
kutiwa saini na Malkia Elizabeth kuwa sheria.
Akiwa
Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama
inavyotoa kwa raia wengine.


Comments
Post a Comment